Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watani wamesimama hapa CAFCL

Kumekucha Mapinduzi Cup! Simba, Yanga Ndani! Watani wamesimama hapa CAFCL

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba na Yanga kila mmoja amepata ushindi katika michezo iliyopita ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba wakiitandika Wydad Casablanca 2-0 Uwanja wa Benjamini Mkapa na Yanga wakitumia dimba hilohilo kumpoteza Medeama mabao 3-0.

Ushindi kwa timu hizo ni wa kwanza msimu huu katika hatua ya makundi ya michuano hiyo baada ya kupitia ukame wa kutoshinda katika michezo mitatu iliyopita.

Wababe hao wa Kariakoo, Dar es Salaam wote wamefikisha alama tano katika makundi yao Simba akiwa kundi B wakati Yanga yeye akitamba katika kundi D baada ya kucheza michezo minne.

Michezo miwili imesalia kwa timu hizo kuipigania nafasi ya kucheza hatua ya robo fainali ya mitanange hiyo, huku matumaini yakiongezeka baada ya ushindi katika michezo iliyopita.

Una maoni usisite kutuandikia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live