Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakiwasha Ligi Kuu ya wanawake

Ligi+kuu+wnwk+pic.png Watakiwasha Ligi Kuu ya wanawake

Mon, 28 Sep 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Mustafa Mtupa MSIMU mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake unatarajiwa kuanza Oktoba japo tarehe hajapangwa hadi sasa. Jumla ya timu 12 ndizo zitakazoshiriki ligi hiyo zimeonekana kufanya usajili wa wachezaji ambao unatarajiwa kusumbua sana kutokana na viwango walivyoonesha msimu uliopita.

Mbali na wachezaji wapya waliosajiliwa kwenye vikosi husika, pia kuna wachezaji wa zamani wa timu hizi ambao pia wanatarajiwa kuwa watakuja kusumbua sana kwa kuangalia pale walipoishia msimu uliopita. Mwanaspoti inakuletea nyota ambao wanatarajiwa kuonyesha kiwango kikubwa kwa msimu huu.

Oppah Clement (Simba Queens)

Miongoni mwa wachezaji waliochangia Simba kuchukua ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu msimu uliopita ambapo alimaliza msimu kwa kufunga mabao 16 na kuwa mmoja kati ya wachezaji wawili wa Simba ambao walifunga mabao mengi. Oppah amekuwa na muendelezo wa kufunga mabao zaidi ya kumi kwa misimu miwili. Kiwango alichoonesha msimu uliopita kinaashiria huenda akawa na makali zaidi katika msimu huu.

Fatuma Mustafa (JKT Queens)

Amekuwa hapewi heshima kubwa huenda kwa sababu aina ya timu ambayo anachezea kutokuwa na kundi kubwa la mashabiki, lakini fundi huyu amekuwa na muendelezo wa kufunga mabao mengi tokea aanze kucheza katika Ligi Kuu, msimu wa 2016-17 alifunga mabao 18, 2017-18 alifunga mabao 25, 2018-19 alifunga mabao 38 na msimu uliopita mabao 31 na amekuwa mfungaji bora kwa misimu miwili mfululizo. Msimu huu pia anatajwa kuwa huenda atasumbua kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufumani nyavu.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz