Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakaoanza Simba ikiikabili Al Merreikh hawa hapa

Simba Kufuru Pic Data Watakaoanza Simba ikiikabili Al Merreikh hawa hapa

Sat, 6 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Thobias SebastianMore by this Author SUDAN

Mazoezi ya mwisho ya Simba yamekamilika muda huu katika uwanja wa Al Hilal ya hapa Khartoum Sudan.

Mazoezi hayo ya Simba ambayo yalifanyika kwa saa moja tu, kuanzia saa 8:30 mchana mpaka saa 9:30 mchana kwa saa za hapa Sudan.

Wachezaji wa Simba hawakufanya mazoezi mengi magumu wala kukimbia bali ni yale machache tena mepesi mepesi.

Miongoni mwa mazoezi ambayo walilifanya walikimbia mbio za mwendo wa kawaida na walizunguka uwanja mara mbili, mazoezi ya viungo, utimamu wa akili na mengine machache.

Zoezi la mwisho ambalo Simba walifanya la kucheza timu mbili na hapo Mwanaspoti lilibaini wachezaji ambao wanakwenda kuanza katika kikosi cha kwanza.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz