Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasudani wamnyatia kipa Azam FC

Aloi Ahmada Vs Kakolanya Ali Ahamada

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Al-Merreikh ya Sudan imetuma ofa rasmi ya kumhitaji kipa wa Azam FC, Ali Ahamada kwa mkopo wa msimu mzima.

Kipa huyo wa kimataifa wa Comoro aliyezaliwa Ufaransa alijiunga na Azam Julai mwaka jana ila amekosa nafasi ya kuanza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza tangu aliposajiliwa kipa mwenzake Mghana, Abdulai Iddrisu.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo ililiambia Mwanaspoti ni kweli viongozi hao wa Sudan wametuma ofa ya kumuhitaji kipa huyo na mazungumzo baina yao yanaendelea chini kwa chini japo muafaka haujafikiwa.

“Ni kweli wameonyesha nia ya kumuhitaji lakini viongozi bado wana wasiwasi akiondoka kutakuwa na upungufu ya mbadala wake kwa sababu ukiachana na Iddrisu ila, Zuber Foba bado hana uzoefu,” kilisema chanzo chetu.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’ alipotafutwa kuzungumzia suala hilo alisema; “Kwa sasa hatuwezi kuzungumzia hilo kwa sababu akili zetu zote ziko kwenye mchezo wa awali wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bahir Dar Kenema (jana), kwa lengo la kuhakikisha tunafanya vizuri ugenini.”

Hata hivyo, Mwanaspoti linatambua licha ya kipa huyo kusafiri na kikosi hicho kilichoenda Ethiopia kwa ajili ya mchezo huo, kuondoka kwake kutategemea uamuzi wake binafsi na hatapata shinikizo lolote kwa viongozi ambao wanampa huduma za kifahari jijini Dar es Salaam na anaendesha gari kali kuliko wachezaji wote nchini akisemekana kulipwa mshahara wa Sh50 milioni kwa mwezi.

Chanzo: Mwanaspoti