Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washambuliaji ni tatizo

A18222258902fb84d445960ee6d60a17 Washambuliaji ni tatizo

Wed, 14 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA wa Mwadui, Khalid Adam amesema safu yake ya ushambuliaji imekuwa ikimuangusha kwa kukosa umakini, ila sasa amepata ufumbuzi wa tatizo hilo.

Mwadui ipo Dar es Salaam ikitarajiwa kumenyana na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Adam alisema siku ambazo ligi imesimama amezitumia vyema kurekebisha mapungufu ya ushambuliaji ili kurudi na kasi mpya.

“Safu ya ushambuliaji imekuwa ikitengeneza nafasi nyingi za kufunga ila umakini ulikosekana ndio maana tumecheza mechi kadhaa za kirafiki kwa ajili ya kufanya marekebisho na kujua matatizo yetu ili kuyafanyia kazi,” alisema.

Hivi karibuni timu hiyo ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Azam Complex.

Kocha huyo alisema wamejipanga vizuri na ana amini wachezaji wake watayafanyiakazi aliyowaelekeza ili kupigania pointi tatu kuanzia mchezo wa kesho na mingine iliyoko mbele yao.

Timu hiyo inayotoka Shinyanga inakiri kuwa ligi msimu huu ni ngumu ikilinganishwa na msimu uliopita kwani kila timu imeonesha ushindani wa hali ya juu.

Mwadui imecheza michezo mitano na kati ya hiyo imeshinda miwili na kupoteza mitatu na ina pointi sita.

Chanzo: habarileo.co.tz