Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasauzi wamuwinda Fei Toto

Fei Totooo.jpeg Wasauzi wamuwinda Fei Toto

Tue, 23 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati kamati ya hadhi za wachezaji ya shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) likisisitiza kuwa Feisal Salum "Feitoto" ni mali ya Yanga SC, klabu ya soka inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini (PSL) Sekhukhune United imeanza mazungumzo na wawakilishi wa kiungo huyo wa timu ya taifa ya Tanzania.

Inasemekana mazungumzo kati ya klabu hiyo pamoja na wawakilishi wa Feisal Salum yameanza na klabu hiyo inamhitaji kiungo huyo ili kuongeza nguvu kwenye kikosi cha timu hiyo.

Sekhukhune United waliomaliza wakiwa nafasi ya saba(7) kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Afrika Kusini wanatumia uwanja wa Peter Mokaba Stadium uliopo kwenye jiji la Polokwane.

Hawa wameanza maboresho ya kikosi chao kuelekea msimu ujao na tayari wameanza mazungumzo na wawakilishi wa Feisal Salum "Feitoto".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: