Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waruka ukuta kuingia Uwanjani wakihofia Ushirikina

Waruka Ukuta Wachezaji wa Lumwana Radiants wakiingia Uwanjani

Sun, 5 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa klabu ya Lumwana Radiants ya Ligi kuu ya Super League ya Nchini Zambia waligoma kutumia njia elekezi ya kuingia uwanjani na kulazimika kuruka ukuta wa uzio kuingia uwanjani.

Hata hivyo juhudi hizo hazikuwasaidia kuepuka kichapo cha 2-1 kutoka Green Buffaloea FC.

Klabu hiyo ilifanya hivyo kuhofia ulozi kutoka kwa wapinzani wao hao, na kuzua taharuki kwa wapenzi wa kandanda.

Katika Msimamo wa Ligi Kuu ya nchini Zambia, klabu ya Lumwana Radiants inakamata nafasi ya 17 kati ya timu 18 zinazoshiriki Ligi Hiyo wakiwa na alama zao 26 baada ya kucheza mechi 26.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live