Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Warembo wavamia kambi Timu ya Taifa England

Wachumba England Warembo wavamia kambi Timu ya Taifa England

Fri, 14 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wake na wachumba wa mastaa wa England wameripotiwa kuwatumia zawadi za vifurushi wachumba wao ikiwa ni siku kadhaa kabla ya mechi ya Jumapili ya ufunguzi wa mashindano ya Euro dhidi ya Serbia.

Vifurushi hivyo viliwekwa kwenye vitanda vya wachezaji kabla ya hawajawasili kwenye kituo chao watakachokuwa wanakitumia muda wote wa mashindano huko Blankenhain.

Ndani ya vifurushi kulikuwa na barua zilizofungwa kutoka ambazo zilikuwa na ujumbe wa kuwatia moyo na mastaa wengine wenye watoto walikuta barua za wa-toto wao wakiwatakia heri kuelekea mashindano hayo.

Pia kulikuwemo na picha za familia, manukato wanayotumia majumbani kwao.

Chanzo kimoja kilisema: “Kila mwanamke alitengeneza sanduku lenye vitu maalum, waliandika barua ambazo zitafunguliwa kwa siku maalum ambazo ndani yake kuna ujumbe wa kuwapa wachezaji nguvu zaidi.

“Pia kuna picha za familia na marafiki ambazo mchezaji anaweza kubandika kwenye ukuta wa chumba chake cha hoteli, midoli na mito iliyotiwa manukato imewekwa pia.”

“Kifurushi kimeundwa ili kuwafanya wajisikie wako nyumbani zaidi muda wote wanapokuwa kambini kwa sababu muda mwingi hatatokuwa pamoja na familia zao na inaelezwa wanaweza wasikutane nao muda wote wa mashindano.”

Katika michuano iliyopita, Gareth Southgate, aliwaruhusu wachezaji kukutana na familia zao kwa siku moja baada ya kumalizika kwa hatua ya makundi lakini hakuna uhakika kama huko Ujerumani pia atawaruhusu wafanya hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live