Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapinzani wa Yanga, mpige mahesabu huko mlipo

Yanga Sc Media Officer Hassan Bumbuli Spge0rsmuoel148ictakf1pod?fit=1200%2C800&ssl=1 Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Yanga, Hassan Bumbuli

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuanza vyema Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa ushindi wa asilimia 100, ndani ya mechi tano za mwanzo, Klabu ya Yanga imetoa tahadhari kwa wapinzani wanaokuja mbele yao wajihadhari na kujipigia mahesabu ya goli ngapi watafungwa.

Yanga ambayo mpaka sasa imecheza michezo mitano ambayo ni;

Yanga vs Kagera wakashinda 1-0, Yanga vs Geita Gold wakashind 1-0, Yanga vs KMC wakashinda 2-0, Yanga vs Azam wakashinda 2-0 na kisha Yanga vs Ruvu wakashinda 3-1.

Sasa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mwasiliano Yanga, Hassan Bumbuli amewaambia wale wote wanaokwenda kukutana na Yanga watazame kwa wakati huo Yanga ipo kwenye kutoa kipigo cha magoli mangapi kisha wajipimie adhabu wanayokwenda kukutana nayo.

"Labda tu niwakumbushe wale wenzetu waliopo katika ligi moja na sisi wajue tu kuwa kadiri tunavyoongeza kasi ya vipigo basi hata ukiwa unakuja kukutana na sisi utambue mapema kwa wakati huo tunaadhibu kwa kiwango cha magoli mangapi"

"Hiyo itakusaidia kuondoa mshangao mwishoni mwa mchezo, na kama upo mbali kukutana na sisi basi ndio hatar zaidi" amesema Bumbuli

"Tulianza na goli moja moja, tumekuja mbili na zitaendelea kwa kila kocha atakavyoona inafaa"

Yanga inaongoza msimamo wa Ligi ikiwa na alama 15 baada ya kushuka dimbani michezo mitano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live