Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapinzani wa Yanga CAFCL watambulisha kocha mpya

Vital O Burundii Wapinzani wa Yanga CAFCL watambulisha kocha mpya

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Vitalo FC ya Burundi imeingia mkataba wa mwaka mmoja na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya BS Dynamik, Haruna Ferouz ikiwa ni katika maandalizi ya Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika na Ligi Kuu nchini Burundi.

Vitalo FC wawakilishi wa Burundi katika Mashindano hayo ya Kimataifa wamepangwa kukutana na Yanga ya Gamondi katika hatua ya awali ya mtoano ya Klabu Bingwa Afrika kwenye droo iliyofanyika leo Cairo nchini Misri.

Miamba hiyo ya Burundi inarejea katika michuano ya Kimataifa baada ya kumaliza muda mrefu bila kushiriki michuano hiyo.

Katika uteuzi huo, aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo Sahabo Parris atakuwa kocha msaidizi chini ya kocha Ferouz.

Mbali ya Vitalo FC, Rukinzo FC watakuwa wawakilishi wa Burundi ngazi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ambapo wamepangwa kukutana na Hoseed FC ya Somalia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live