Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapinzani wa Yanga CAF sio kinyonge aisee!

Asas Fc 2023 07 25T163938.jpeg Wapinzani wa Yanga CAF sio kinyonge aisee!

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ina kibarua cha kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga la kimataifa.

Ni katika Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga itakuwa na kazi ya kupeperusha bendera ya Tanzania.

Katika hatua ya awali Yanga inatarajiwa kumenyana na Association Sportive d’Ali Sabieh Djibouti Télécom ambayo haipo kinyonge uwanjani.

Wapinzani wa Yanga ni klabu kutoka Djibouti inashiriki kwenye ligi kuu ya Djibouti Premier League.

Klabu ya As Ali Sabieh imeanzishwa mwaka 1991 na inamiliki uwanja wa El Hadj Hassan Gouled Aptidon.

Uwanja wa wapinzani wa Yanga kimataifa una uwezo wa kuingiza mashabiki 20,000 . Asas wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya ndani “Djibouti Premier League” mara saba na Djibouti Cup mara tatu ndio klabu iliyofanikiwa zaidi nchini humo.

Yanga ina kazi ya kupata ushindi kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: