Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapinzani wa Yanga CAF hakuna kulala

Marumo Gallants.jpeg Wachezaji wa Marumo Gallants

Sat, 6 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati klabu ya Yanga ikiwa mchezo wao wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho Azam dhidi ya Singida Big Stars kusogezwa mbele, wapinzani wao kwenye nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Marumo Gallants wanaendelea na mechi zao kama kawaida.

Yanga iliandika barua rasmi ya kuomba mchezo wao wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Azam uliotakiwa kuchezwa Mei 7 usogezwe mbele na TFF tayari imeweka Rasmi kuchezwa tarehe 21 Mei 2023 kwa lengo la kupisha maandalizi kwa ajili ya mechi dhidi ya Marumo.

Marumo Jumatano ya wiki hii ilikuwa na mechi (Ugenini) ya Ligi Kuu dhidi ya Maritzburg na mchezo huo ulimalizika kwa sare 2-2.

Yanga ilicheza mchezo wake wa Ligi Kuu jana (Alhamis) dhidi ya Singida Big Stars (Ugenini) na ilishinda 2-0.

Wakati Yanga ikiwa haina mchezo wowote kwa sasa baada ya mechi yao kusogezwa, Marumo kesho itakuwa na mchezo mwingine mgumu wa Ligi Kuu dhidi ya Mamelod Sundowns.

Sare ya 2-2 ambayo Marumo ilipata dhidi ya Maritzburg inawafanya wawe nafasi ya 14 ikiwa na pointi 29. Mchezo wao na Mamelod ni muhimu kwa timu zote mbili kwani Mamelod inayoongoza Ligii kiwa na pointi 66 inahitaji ushindi kujiweka sehemu nzuri kwani nafasi ya pili ni Orlando Pirates ikiwa na pointi 50 na wote wamecheza mechi 28.

Wakati huo huo Marumo yenyewe inaepuka kuwa kwenye hatariya kushuka daraja kwani nafasi ya 15 ni Chippa United ikiwa na pointi 29 huku nafasi ya mwisho (16), Maritzburg ina pointi 26.

KERR AFUNGUKA

Kocha mkuu wa Marumo Gallants, Dylan Kerr amesema mechi zote ni muhimu kwao na kila mechi ina falsafa yake.

“Kweli tuna mechi ngumu mbili kabla ya kukutana na Yanga lakini hilo sio baya kwetu kwa sababu tunatakiwa kucheza,” amesema Kerr.

Kerr ameongeza na kusema;”Mechi za Ligi na nusu fainali ya Caf huko ni vitu viwili tofauti,, matumaini yangu nakuja Tanzania na kucheza mchezo mzuri.”

Yanga na Marumo zitacheza mchezo wao wa kwanza hapa nchini Mei 10 kisha watarudiana nchini Afrika Kusini Mei 17

Chanzo: Mwanaspoti