Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapenzi wawili wauawa kwa kuchinjwa kisa wivu

PANGA Wauawa kwa kuchinjwa wivu wa mapenzi

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni wapenzi Katalina Juma (21) na Athanas Alyen ( 23) wakazi wa Kata ya Kabungu, Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wamekutwa wakiwa wameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali, huku chanzo kikidiwa ni wivu wa mapenzi.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Oktoba 19, 2023 katika Kitongoji cha Imbambe, Kijiji Cha Kagwira, Kata ya Kabungu, ambapo marehemu hao wamekutwa wamefariki dunia kwa kuchinjwa na kutupwa pembezoni mwa barabara.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kagwira, Shila Benedicto amesema marehemu hao walikutwa na madhila hiyo wakiwa njiani kurudi nyumbani wakitokea Kijiji cha Kabungu walikokuwa wakifanyia shughuli zao.

Akithibitisha kutokea tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani amesema wanawashikilia watu wawili kwa ajili ya mahojiano, huku akieleza kuwa tukio hilo lina sura ya wivu wa kimapenzi kwa kuwa wamebaini mmoja wa marehemu alikuwa akiwasiliana na watu ambao walikuwa wapenzi wake.

Kamanda ngonyani amesema Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo na mara utakapokamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live