Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanyama hataki kuondoka Marekani

Victor Wanyamaaaaa Victor Wanyama

Thu, 1 Sep 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Nahodha wa zamani wa Harambee Stars, Victor Wanyama, hataki kwenda Italia au Uturiki ila anataka kuendelea kupiga soka lake la kulipwa Marekani katika Major League Soccer (MLS).

Kiungo huyo atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu na tayari ameweka wazi nia yake ya kutaka kuendelea kupiga soka lake kwenye ligi hiyo.

Wanyama anayeichezea klabu ya CF Montreal alisema bado hajaanza mazungmzo ya mkataba mpya na klabu hiyo lakini amesisitiza angelipenda kuendelea kuishi kule.

Kiungo huyo alihamia Canada iliko CF Montreal Machi 2020 akitokea Totteham Hotspurs ya England.

Mkurugenzi wa klabu hiyo, Olivier Renard, wiki chache zilizopita alifichua bado klabu haijaanza majadiliano ya kurefusha mkataba na Wanyama.

“Bado hatujazungumza ila sote tunajua hali iliyoko mbele yetu. Ndani ya siku chache zijazo tutajua nini kitakachotokea. Timu kadhaa zinazidi kuboreka na ligi inazidi kuwa yenye ushindani. Dhamira yangu kwasasa ni kuendelea kucheza huku,” alisema Wanyama ambaye mkataba wake na CF Montreal umesalia na miezi minne tu.

Tayari Wanyama ameanza kuhusishwa na tetesi za kuhamia Uturuki au kujiunga na ligi kuu ya Italia, Serie A, kwenye dirisha dogo la usajili Janauri mwakani.

Awali, Renard alisema kuna baadhi ya mambo wanayopaswa kujadili mwanzo kabla ya kuamua kama atamwongezea mkataba au la.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz