Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne wakoleza moto Tabora Utd

Tabora Wanne Wanne wakoleza moto Tabora Utd

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Tabora United, Goran Kopunovic amesema nyota wanne wa kikosi hicho waliokuwa wanasumbuliwa na majeraha wamerejea mazoezini kujiunga na wenzao kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC.

Wachezaji hao ni John Noble na Erick Okutu waliopata majeraha wakati wa mchezo wa timu hiyo dhidi ya Namungo ulioisha kwa sare ya bao 1-1 Februari 11 na Kelvin Kingu ambaye amekuwa nje kwa zaidi ya miezi sita baada ya kutenguka mguu.

Nyota mwingine ni Mkongomani, Lumiere Banza Kalumba aliyekuwa na changamoto mbalimbali za kifamilia jambo lililopelekea kushindwa kujiunga na kikosi hicho wakati kilipokuwa kambini mkoani Shinyanga kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Mwanaspoti, Goran alisema urejeo wa wachezaji hao ni jambo nzuri kwao kutokana na umuhimu wao kikosini na isitoshe michezo 15 ya mzunguko wa pili wanahitaji kufanya vizuri zaidi ya walivyofanya awali licha ya ushindani uliopo.

“Kupata pointi moja kati ya sita katika michezo yetu miwili tuliyocheza haitoshi na haituweki kwenye mazingira mazuri ya kiushindani, hivyo bado tunatakiwa kufanya zaida ya sasa kwa sababu malengo ni kumaliza nafasi tano za juu,” alisema. Goran aliongeza, nyota mpya wa timu hiyo Mkongomani, Nelson Omba Munganga aliyetokea klabu ya DC Motema Pembe ana imani kubwa kwake katika kukisaidia kikosi hicho kutimiza malengo hayo kutokana na uzoefu alionao katika timu alizochezea.

“Baadhi ya wachezaji wa kigeni tuliowasajili dirisha dogo wameshindwa kuonekana kutokana na kukosa vibali vyao vya kazi, ingawa muda wowote kuanzia sasa wataanza kucheza kwa sababu taratibu zote zinaendelea vizuri na ziko karibu kukamilika.”

Katika mechi ya duru la kwanza baina ya timu hizo, Tabora ilipokuwa ikitumia jina la Kitayosce ilikandikwa mabao 4-0 ikiwa na wachezaji nane uwanjani, kabla ya wachezaji wawili ‘kujivunja’ na mchezo kuvunjika ikichezwa kwa dakika 18 tu, hivyo mechi ya kesho wenyeji watakuwa na kazi ya kusahihisha makocha kudhibitisha iliotewa tu, pale Chamazi.

Chanzo: Mwanaspoti