Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanigeria wapishana Tabora Utd

John Noble John Noble

Sun, 28 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Tabora United iko katika hatua za mwisho za kukamilisha uhamisho wa kipa Victor Sochima kutoka Rivers United ya Ni-geria akipishana na Mnigeria mwenzake John Noble aliyekuwa akiidakika aliyetua Fountain Gate kwa ajili ya msimu ujao.

Sochima yupo katika mazungumzo na Tabora United baada ya Noble aliyetua nchini Julai 31, mwaka jana akitokea Enyimba kuondoka katika kikosi hicho na kujiunga na Fountain Gate (zamani Singida Fountain Gate).

Akizungumza na Mwanaspoti, Sochima alisema ni mapema kuzungumzia suala hilo ingawa mambo yatakapokamilika ataweka wazi, japo shauku yake kubwa ni kuona siku moja anacheza soka nchini Tanzania kwa sababu limezidi kupiga hatua barani Afrika.

“Nimekuwa na mazungumzo na klabu nyingi, lakini bado sijafikia muafaka wa kuamua ni wapi nitachezea kwa msimu ujao. Hata hapa Rivers United wanahitaji niendelee kubaki, hivyo acha tusubiri hadi muda utakapofika mashabiki watajua,” alisema.

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Tabora United, Richard Abwao alisema kwa sasa viongozi wana mambo mengi ya kufanya, ikiwemo kuhakikisha wanalipa fedha wanazodaiwa wachezaji mbalimbali walioshtaki Fifa ili wafunguliwe kwa ajili ya usajili wa msimu ujao. “Lengo letu la kwanza lilikuwa kuhakikisha kwanza timu inabaki Ligi Kuu Bara na tunashukuru tumefanikiwa kwa hilo. Kwa sasa tunapambana na madeni tunayodaiwa na Fifa kisha baada ya hapo ndipo tutaanza kuzungumza mambo mengine,” alisema.

Wakati Abwao akizungumza hayo, Mwanaspoti linatambua kwamba Tabora imeanza harakati za usajili kimyakimya huku kipa huyo aliyewahi kuchezea timu mbalimbali zikiwamo Jigawa na FC Heartland zote za Nigeria akiwa ndiye chaguo la kwanza.

Uhamisho huo utakapokamilika utamfanya Sochima kuwa mchezaji wa pili kutoka Rivers United kusajiliwa na timu, baada ya hivi ka-ribuni kuona Simba ikiinasa saini ya aliyekuwa kiungo nyota wa kikosi hicho, Augustine Okejepha.

Chanzo: Mwanaspoti