Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake nchini washauriwa kushiriki Michezo ya Jadi

Wanawake Jadi Wanawake nchini washauriwa kushiriki Michezo ya Jadi

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanawake nchini wameshauriwa kushiriki michezo hususani ya jadi kwani ushiriki wa michezo hiyo si kwa wanaume pekee

Wakizungumza kwenye michezo ya bandari Interpot mjini Morogoro, baadhi ya wachezaji wa michezo ya jadi wamesema kuwa wanawake wanatakiwa kuacha dhana potofu kwani michezo hiyo ni kwa watu wa jinsi zote hivyo wanawake wanatakiwa kujitokeza kwa wingi.

Ushiriki wa wanawake katika michezo ya jadi kwenye mashindano ya 17 ya bandari ambayo yamekuwa yakitawaliwa na wanaume huku bingwa mtetezi ni timu ya shirika la bandari Zanzibar ZPC ni kwa mara ya kwanza ambapo ushindani kwa wanawake ni kiwango kikubwa .

Michezo hiyo ya siku nane ipo katika siku ya pili ikishirikisha zaidi ya wanamichezo 760 kutoka timu nane za bandari za TPA na wadau wake zikiwemo timu za shirika la bandari Zanzibar- ZPC na kampuni ya huduma za Meli - MSCL na itafikia tamati tarehe 30 Oktoba, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live