Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake changamkieni mafunzo ya TFF

Ad4c74b8c4f09c9fa894efce838e6641 Wanawake changamkieni mafunzo ya TFF

Sat, 19 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF), Jumanne ya wiki hii lilizindua kozi ya uongozi na utawala kwa wanawake na leo inafi kia tamati.

Kozi hiyo ya siku tano ina lengo la kuwajengea uwezo wanawake katika soka kwani soka ya wanawake inakua siku hadi siku.

Washiriki wa kozi hiyo kwa Dar es Salaam walikuwa 32, ambao ni viongozi wa klabu na wadau wa soka ya wanawake.

Mara kadhaa, TFF imekuwa ikifanya kozi ya aina hii kwa wanawake wapenda soka, safari hii kwa mujibu wa rais wake Wallace Karia, lengo ni kuifanya katika mikoa 10 ikiwemo Mwanza, Tanga na Simiyu.

Katika uzinduzi huo, Karia aliwaambia waandishi wa habari kuwa lengo ni kupata wanawake 300 katika mafunzo hiyo. Si idadi ndogo kwa kuanzia na katika hili tunaipongeza TFF kwa kuamua kutoa mafunzo kwa wanawake.

Dunia ya sasa soka ya wanawake inashika kasi na Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoipa kipaumbele hivyo sio vibaya kama watapatikana viongozi na kuwaongoza wenzao.

Imekuwa kawaida wanaume kuongoza soka la wanawake kwenye mambo mbalimbali, lakini wanawake wakipatiwa mafunzo hakuna shaka kuwa wataweza kujiendesha wenyewe.

Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred alisema kwenye uzinduzi huo kuwa wakimaliza mafunzo hayo kwa viongozi watafanya kazi za makocha, pongezi kwa hilo hakika wanahitajika makocha wa kike kwa ajili ya timu za wanawake hasa kwa vile siku hizi kumekuwa na ligi na michuano mbalimbali ya wanawake.

Tumeshuhudia timu mbalimbali zikiongozwa na makocha wa kiume, hivyo mafunzo hayo ya ukocha pia yatakuwa msaada mkubwa kwa wanawake nao kuzinoa timu za wanawake.

Tuna imani kama ilivyofanikiwa kwenye waamuzi wa kike, bila shaka na kwenye uongozi na makocha pia itafanikiwa.

Ni jambo zuri kuamua kuwaendeleza wanawake kwani elimu hiyo bila shaka itakwenda mbali zaidi na kuinua wanawake wengine.

Mwito kwenu wanawake kujitokeza kuifanya kozi hiyo inapofika kwenye mkoa husika, wanawake mjitokeze kwa wingi ili kuongeza idadi yenu kwenye mpira wa miguu wa wanawake

Chanzo: habarileo.co.tz