Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanasoka hawa ni burudani juu ya burudani

Skudu Raha Wanasoka hawa ni burudani juu ya burudani

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Unamkumbuka Eric Cantona, nahodha wa zamani wa Manchester United? Fabien Barthez je? Aliidakia miamba hiyo ya Ligi Kuu England kuanzia mwaka 2000 hadi 2004.

Unajua wanafanya nini sasa hivi? Mmmoja ni dereva wa mbio za Langalanga (Barthez) na Cantona anacheza filamu huko kwao Ufaransa.

Hao ni kati tu ya mastaa ambao mbali na kucheza soka, wana fani nyingine na wanaziweza hasa.

Hapa nchini pia kuna nyota ambao mbali na kucheza soka, kuna fani nyingine wanazimudu na kama sio soka basi ungewakuta au utawakuta huko.

Kiungo wa zamani wa Simba na Yanga, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima amewahi kuingia kwenye Bongo Movie na aliigiza kwenye filamu ya The Ring na wengi walishangazwa na ujuzi wake.

Mbali na kuigiza pia anajua kuimba na aliwahi kukiri ni mkali wa hip hop na amesharekodi baadhi ya nyimbo.

Baadhi ya mastaa kwenye soka ni madansa, wapiga vyombo vya muziki kama gitaa na waimbaji.

Mwanaspoti linakuchambulia mastaa hao ambao ukiwatoa kwenye soka, hawalali njaa kwani fani nyingine zitawaokoa.

MFUKO-KAGERA SUGAR

Beki wa Kagera Sugar, Abdallah Mfuko licha ya umahiri wake wa kukaba na anavyoonyesha sura ya kazi uwanjani, ukimkuta anapiga gitaa na kuimba baadhi ya nyimbo za wasanii kama za Mbosso, Christian Bella na Ali Kiba, itakushangaza sauti yake ya kumtoa nyoka pangoni.

Amewahi kusema kuimba na kupiga gitaa ni starehe yake nje ya soka na huwa anapenda kukaa sehemu utulivu kwani ndiyo mistari inatiririka yenyewe.

“Mara nyingi wachezaji wenzangu ndio wanapenda sana kuona naimba nikiwa kambini, ingawa si mara zote nawakubalia, kiukweli ningeamua kuwekeza nguvu wengi wangejua upande wangu wa pili,” anasema.

SKUDU- YANGA

Winga wa Yanga, Skudu Makudubela aliyesajiliwa kutoka Marumo Gallants ya nchini kwao Afrika Kusini, hadi sasa kacheza mechi tatu dhidi ya Ihefu (dakika 57), Singida Big Stars (dakika 18) na Simba dakika sita. Mbali na soka ni fundi wa kunengua.

Julai 22, wakati Yanga inafanya utambulisho wa mastaa wake wa msimu huu, alitambulisha kipaji chake kingine nje ya soka, alionyesha ufundi wa kucheza Amapiano ambayo ni maarufu zaidi nchini kwao.

MSUVA -JS KABYLIE

Staa Mtanzania anayekipiga JS Kabylie ya Algeria, aliwahi kupitia kwenye kituo cha kukuza vipaji cha THT, hivyo ikitokea kafunga bao alikuwa anashangilia kwa kunengua, hivyo ni kipaji chake kingine nje na soka.

Msuva ambaye aliwahi kuzichezea Azam FC (2010/11),Moro United FC (2011/12), Yanga (2012-2017), Difaâ El Jadida (2017-2020),Wydad AC (2020/21) na Al-Qadsiah FC (2022/23), aliwahi kusema baada ya plani A ya soka kutiki, akaweka nguvu huko, akisisitiza haimzuii kunengua kwani ni kitu anachokipenda.

FETTY DENSA -SIMBA QUEENS

Majina kamili anaitwa Fatuma Issa, alipachikwa jina la utani la Fetty Densa kutokana na umahiri wake wa kudansi na amekuwa kivutio kwa watu mbalimbali wanaomfuatilia kwenye mitandao yake ya kijamii, kwenye kandanda nako siyo wa mchezo mchezo amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Simba Queens na utambulisho wake ni kucheza akiwa amevaa hijabu.

MUSONDA -YANGA

Straika wa Yanga, Kennedy Musonda nje na ufundi wake uwanjani na kwa msimu huu anamiliki mabao mawili aliyofunga dhidi ya JKT Tanzania na Simba, lakini inaeelezwa ni mwana kwaya mzuri wa kanisani kwao na waliowahi kumshuhudia kwenye anga hizo, wanakwambia akianza kuabudu anakuwa na upako unaoweza kumshawishi mtu kuachana na dhambi.

HUKU MAJUU BAADHI YAO

Ukiachana na wanasoka wa Tanzania, huko majuu wapo wanaojua kuimba, huko wengine wamerekodi kabisa, wafuatao ni baadhi yao tu.

Memphis Depay

Fowadi za zamani wa Manchester United na Barcelona ni mmoja ya wanasoka ambao wanafahamu mziki. Mwaka 2017 alianza kuingia katika tasnia ya muziki aina ya kufoka foka (Hop-Hop) na alitoa ngoma yake ya ‘LA VIBES’ wakati alipokuwa mapumzikoni huko Los Angeles, Marekani. Katika video ya nyimbo hiyo alimjumuisha mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya Uholanzi, Quincy Promes. Nyimbo nyingine alizotoa “Fall Back”, “No Love” na “From Ghana”.

RAFAEL LEAO

Beki wa AC Milan na timu ya taifa ya Ureno mara nyingi anapokuwa mapumziko anapenda kwenda studio kwa ajili ya kuimba nyimbo za kufoka kufoka (Hip-Hop) pia anapokuwa studio anakuwa na washakaji wakiimba kwa kutumia lugha ya Kireno. Nyimbo za beki huyo ambazo ametoa mpaka sasa Way 45, Ballin, Stelip Beatz, na Uncle Yankee.

ALLISON BECKER

Licha ya kuwa kipa hatari duniani, nyota huyo wa kimataifa wa Brazil ni mwimbaji mzuri sana.

Anaitumikia Liverpool anapenda kuimba nyimbo za aina ya rock zinazopendwa sana huko Marekani, aliwahi kushirikiana na mwanamuziki kutoka Jiji la Liverpool, Jamie Webste

Chanzo: Mwanaspoti