Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanasema tumefungiwa? Tutawashangaza usajili ujao - Ally Kamwe

Ally Kamwe 89 Ally Kamwe.

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa usajili mpya ujao utakuwa baab'kubwa na watasimamisha nchi kwani Rais wa Klabu hiyo, Eng. Hersi Said ameshaanza kufanya mazungumzo na wachezaji wapya kwa ajili ya kupata saini zao.

"Nimeona watu wanasema kuwa Young Africans tumefungiwa kusajili kwahiyo hatutaruhusiwa kusajili wachezaji hapana haipo hivyo watu hawajaelewa.

"Sisi tunadaiwa madai ya wachezaji kama Lazarous Kambole hivyo tunamlipa mchezaji huyo kwa awamu na pale tutakapomaliza deni tutafunguliwa kusajili.

"Na sisi tuna uhakika wa kulipa deni hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi kwani tukikamilisha tu tunafunguliwa kusajili,utaratibu ndio upo hivyo.

"Sasa kunawatu wasiotutakia mema wanazusha kuwa ndio haturuhusiwi tena kufanya usajili tumefungiwa, niwaambie kuwa tutawashangaza kwenye usajili ujao.

"Tupo makini sana katika usajili na tunachokifanya ni kuanza kuangalia na kufanyia kazi mapendekezo ya awali ya Benchi la Ufundi katika usajili wetu kuelekea msimu ujao, tunataka kuendelea kuwa wafalme wa soka la nchi hii na kuweka rekodi Barani Afrika.

"Niwaambie kuwa tutawashangaza watu kwenye usajili ujao, kwa sababu tunahitaji msimu ujao tuendelee kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya ndani na kimataifa, wasubiri kuona kile viongozi wanachofanya," amesema Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live