Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanapanda ndege sana hawa Simba

Simba Noti Pic Data Wanapanda ndege sana hawa Simba

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Ramadhan EliasMore by this Author UKISIKIA uzoefu basi Simba kwa sasa ina uzoefu. Msimu huu imeonekana kuwa moto Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni msimu wa tatu baada ya 2018/19 kufika robo fainali kabla ya 2019/20 kutolewa hatua za awali.

Huenda moto ilionao mwaka huu unachagizwa na moto waliopitia misimu miwili mfululizo hapo nyuma kwani wajuzi hunena ‘ili Dhahabu iwe, lazima ipite kwenye Moto’ na Wekundu hao wa Msimbazi misimu miwili hiyo waliyopita basi moto waliupata ndio maana nao sasa wako moto.

Achana na habari za msimu wa 2018/19 kufungwa jumla ya bao 12 ugenini kwenye michuano hiyo hatua ya makundi wakipigwa 5-0 na Al Ahly, 5-0 tena na AS Vita pale DR Congo, pia wakapokea 2-0 kutoka JS Saoura pale Algeria lakini walikaza na kutusua kundi hilo kwani waligeuza uwanja wa Taifa kwa sasa Mkapa kuwa machinjio yao na kuwachinja wote hao na kutinga robo fainali.

Msimu uliofuata (2019/20) walitepeta. Ni Luis Miquissone huyu huyu aliyewasulubu Al Ahly juzi kati kwa Mkapa, ndiye aliwafungashia virago msimu huo akiwa na UD Songo hatua ya awali kabisa kwenye mtoano wakitoa suluhu (0-0) nchini Msumbiji na kutoa sare ya bao 1-1 kwa Mkapa.

Bao la UD Songo lilifungwa na Miquissone dakika ya 12, huku Simba wakisawazisha kwa penati dakika za lala salama (87) kupitia kwa Erasto Nyoni matokeo yaliowaondosha Simba na UD Songo kusonga mbele kwa faida ya bao la ugenini.

Hayo yote yalikuwa mapito magumu Simba waliyopitia wakati wakijijenga kuwa Simba wa sasa aliyemfunga AS Vita bao 1-0 ugenini kwenye dimba lile lile alilopigwa tano misimu miwili iliyopita na anayemfunga Ahly 1-0 kwa Mkapa na kucheza soka safi la kuvutia bila kupaki basi.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz