Mchambuzi wa masuala ya soka nchini Tanzania, Jemedari Said Kazumari amesema kuwa watu wanaoumia na dili la kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama kujiunga na Yanga SC ni wengi.
Chama anatajwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja na Yanga baada ya kutamatika mkataba wake ndani ya Simba huku ikidaiwa kuwa amegoma kuongeza mkataba kutokana na kushindwa kufikia makubaliano na viongozi wa klabu hiyo ambayo ameitumikia kwa misimu mitano na nusu.
"Wanaoumizwa na taarifa za Clatous Chama kugoma kuongeza mkataba Simba SC na kujiunga na klabu ya Yanga ni wengi.
"Linalojulikana ni kuwa Simba itang’oa yeyote. Sidhani kama wageni watazidi watakao baki watazidi 3 katika usajili ujao.
"Kwa maana watakuja wapya saba (7) au tisa (9) kulingana na mahitaji ya kocha mpya mwenye asili ya Afrika na Ulaya. Hapa ndani pia kisu kinaendelea kuchanja, Wanaookota wala wasijisifie saaana.
"This time is Really, Chama is also gone. Habari za uhakika atacheza na Pacome na Aziz Ki timu moja bado utambulisho tu zikiisha hizi figisu za madeni yaliyokubuhu ya FIFA," amesema Jemedari Said.