Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaotamani anachofanya Nyoni wafanye haya

GH7oE 1a4AAdlEO.jpeg Erasto Nyoni

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiraka wa Namungo FC, Erasto Nyoni ambaye umri wake wa pasipoti ni miaka 35, amesema mchezaji kucheza kwa kiwango cha juu kwa muda mrefu kupo ndani ya uwezo wake kama atazingatia na kuacha vitu vinavyoweza kuua kipaji chake.

Jambo la kwanza alilolitaja Nyoni alisema mchezaji ni lazima awe na uhakika wa chaguo la kazi yake kwani hiyo itamsaidia pale anapokutana na changamoto kupambana nazo na hazitamuondoa kwenye mstari wa kupambania anachokiamini.

"Shida inakuja mchezaji akipata jina, anajisahau na kuanza kutembea na upepo wa mashabiki badala ya kuweka nguvu kwenye majukumu yake, hilo limewaondoa wengi mchezoni," alisema Erasto ambaye pia alicheza katika klabu ya Simba na Azam.

Nyoni ambaye anaongoza kwa kucheza mechi 107 za timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', alisema kinachomfanya acheze kwa muda mrefu na wengi kutamani kufikia mafanikio yake ni nidhamu.

"Kwanza napenda soka, lipo kwenye damu yangu, ndio maana silazimishwi kujitunza, kuzingatia programu za makocha, kufanya mazoezi binafsi nje ya timu, kupumzika na kupunguza muda mwingi wa kuzurura mtaani," alisema na kuongeza;

"Nina uwezo wa kucheza zaidi ya nafasi moja, endapo kama nitakuwa siheshimu kazi, siwezi kumudu majukumu, nayamudu kwa sababu najituma na nilichagua mpira iwe sehemu ya kukuza kipato changu, sikulazimishwa.

"Vijana wana vipaji vikubwa na wakiamua kuweka nguvu zao kazini tutawaona wakifanya makubwa ndani na nje, itakuwa kama wageni ambao wanaimbwa kila siku na wao wataimbwa, waamue kujituma."

Chanzo: Mwanaspoti