Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wanafunga hivi Ligi Kuu leo

Yanga Mashabiki Z Wananchi wanafunga hivi Ligi Kuu leo

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Young Africans SC, umeweka wazi viingilio vya mchezo wao wa leo Jumanne dhidi ya Tanzania Prisons ambapo cha chini kabisa ni Tsh 5,000.

Mchezo huo ni wa kuhitimisha msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2023-2024 utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni. Kumbuka mzunguko wa kwanza Yanga waliifunga Tanzania Prisons magoli 2-1 nyumbani kwao.

Viingilio hivyo vipo vya aina tatu ambapo VIP A ni Tsh 20,000, VIP B Tsh 10,000 na Mzunguko Tsh 5,000.

Wananchi tayari wameshakabidhiwa ubingwa na leo watakwenda Chamazi kuufunga msimu kibabe wakiwa na kombe lao la Ligi Kuu ya NBC, hivyo Wananchi wanahizimwa kwenda uwanjani kwa wingi kuendeleza Party la Mabingwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live