Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi hawana muda wa kupoteza

Pacome Faridmm Wananchi hawana muda wa kupoteza

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Young Africans SC, Walter Harson, amezungumzia maendeleo ya kikosi cha timu kipindi hiki ambacho Ligi Kuu ya NBC imesimama, huku akibainisha kwamba, wikiendi kutakuwa na mchezo wa kirafiki.

Harrison amesema: “Maandalizi kuelekea urejeo wa ligi ambao unasubiria ratiba itakayotangazwa na Bodi ya Ligi, kwa Klabu ya Young Africans yanaendelea vizuri na mpaka sasa hivi timu ipo katika maandalizi, mazoezi yanafanyika kwa ratiba tofauti.

“Wiki iliyopita tulikuwa na ratiba ya kutengeneza miili sawa, baada ya hapo, wiki hii tumeendelea kufanyia kazi mazoezi ya uwanjani kimbinu kwa kiasi kikubwa na tumekuwa na vipindi viwili vya mazoezi kwa baadhi ya siku asubuhi na jioni, siku nyingine tunafanya mara moja.

“Yote hayo ni kuhakikisha tunarejesha wachezaji wetu kwenye ubora wao na mwisho wa siku ligi itakaporejea tuhakikishe tunaendeleza malengo yetu ya msimu huu ambayo ni kuhakikisha kwamba tunaenda kutetea taji letu la Ligi Kuu ya NBC.

“Hali iko hivyo katika kikosi chetu na tunategemea kuwa na michezo ya kirafiki wikiendi ambayo itakuwa ya ndani, hatutaruhusu mtu yeyote hii ikiwa ni kuamuliwa na kocha kwa sababu mbalimbali za kimbinu ambazo anazifanyia kazi sasa hivi. Hivyo tunategemea kuwa na michezo hiyo ya kirafiki.

“Baada ya hapo wiki ijayo tutaendelea na mazoezi na tunategemea wachezaji ambao watakuwa wametoka Timu ya Taifa ya Tanzania pamoja na Zambia kwa maana ya Kennedy Musonda na wenzake Watanzania watakuwa wamerejea na kuweza kuongeza idadi kwenye kikosi kabla ya kusubiria ratiba yenyewe ya ligi itakavyotoka na kujua tunaanzia wapi kuweza kutekeleza malengo yetu ya kutetea taji letu la Ligi Kuu ya NBC.”

Ikumbukwe kwamba, Ligi Kuu ya NBC imesimama tangu mwishoni mwa 2023 kupisha michuano ya AFCON iliyoanza Januari 13, 2024, ambapo baada ya Taifa Stars kuishia hatua ya makundi, ligi hiyo inatarajiwa kuendelea hivi karibuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live