Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanamkosea heshima Fred

Wanamkosea Fred Easd Wanamkosea heshima Fred

Tue, 23 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kumekuwa na maneno mengi sana kuhusu usajili wa dirisha dogo kwa timu mbalimbali japo kwa Simba Sc ndio imekuwa muhanga wa maneno hayo.

Mwanzoni hata mimi niliingia mkenge kwamba wamekosea sana, ila baada ya kufanya tafiti kadhaa nikagundua Simba wamepatia kwa Fred Koublan. Sio rahisi sana kuelewa kwa haraka haraka kama hutatuliza kichwa chako na kuweka pembeni maneno yanayosemwa juu ya mchezaji huyo.

Kwa mchezaji ambaye anaweza kuwa na zaidi ya magoli 20 kwa msimu anakuaje mbovu??

Ametoka ligi ya Zambia akiwa na magoli 14, amekuja Simba na amefunga magoli 7 mpaka sasa (matatu kwenye crdb federation na manne kwenye ligi nbc premier) kwa tafsiri nyingine ni kwamba ndani ya msimu huu amefunga magoli 21.

Hiki ni kiwango cha top striker anayestahili kucheza ligi ya Tanzania. Bahati mbaya yake ni kwamba ameingia Simba katika msimu ambao hauonekani kuwa wa mafanikio hivyo kumezwa na hali ya ukosefu wa vikombe pale Msimbazi.

Katika timu ambayo ameingia dirisha dogo na sasa anashika nafasi ya tatu kwa wafungaji wa Simba (nyuma ya Chama na Saidoo wenye goli 7) huwezi kusema huyo sio striker.

Pengine kwa vile hana vyenga na kanzu, pengine hana staili nzuri ya kushangilia labda ndio maana anaingia kwenye orodha ya wachezaji “wabovu”.

Lakini kwangu Mimi mchezaji anayeweza kufunga magoli 20 kwa msimu huyo ni top striker…. Mpaka sasa mtu mwenye goli 21 kumuita mbovu yataka ujasiri.

Kwanini wenye nafasi ya kumtetea wamekaa kimya hawasemi huyu ni striker hatari na wataje namba zake? Hata Mimi sijui kwanini. Kwanini watu wanaaminishwa kuwa pale hakuna striker na wao wameamini? Hata Mimi sijui.

Ila kama atavuka mtaa wa pili, au akatembea tembea mpaka Mbande basi watesi wake ndio watashtuka na kushangaa kumbe “walifuata mkumbo” katika “kumbagaza” ndugu Fred.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live