Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi ndio kiboko ya Mayele

Mayelo No Goal Wanajeshi ndio kiboko ya Mayele

Thu, 26 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kinara wa upachikaji wa mabao Yanga, Fiston Mayele amekwama kuifunga Ruvu Shooting msimu wa pili sasa tangu amejiunga na Yanga akitokea As Vita ya Congo, lakini ishu ni kwamba hata Prisons hawajafungwa na jamaa huyo.

Wakati Mayele akishindwa kufanya hivyo baada ya kuzifunga timu nyingine za Ligi Kuu Bara akibakiza Simba ambayo bado wana mchezo nayo mzunguko wa pili pia vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga kucheza mechi 20 kwa kufunga kila mchezo rekodi hiyo imevunjwa na Ruvu Shooting ambao wamekubali kipigo cha bao 1-0, bao wakijifunga wenyewe.

Yanga imepata ushindi huo na kuendelea kujiimarisha kileleni wakifikisha pointi 56, wakiwaacha watani zao Simba pointi sita wote wakiwa wamecheza mechi 21.

Kipindi cha kwanza Yanga walianza kwa kutulia wakisaka bao la kuongoza lakini uimara wa Ruvu Shooting uliwafanya washindwe kupenya kutokana na timu hiyo kuingia kwa kujilinda wote wakirudi nyuma.

Pamoja na timu nzima kurudi nyuma haikuwazuia Yanga kuendelea kupeleka mashambulizi langoni mwa Ruvu ambao waliongeza ulinzi zaidi kutokana na wapinzani wao kulazimisha kusaka bao la uongozi.

Yanga walitumia dakika 33 kupenya ukuta wa timu hiyo baada ya Djuma Shabani kupenyeza pasi nzuri akimtengenezea nafasi Musonda ambaye aliukosa mpira ambao uliunganishwa kambani moja kwa moja na Mpoki Mwakinyukwe.

Bao hilo liliwaamsha Yanga ambao walionyesha nia ya kusaka bao lingine na walipata kona tatu kipindi cha kwanza huku Ruvu Shooting wakipiga kona moja iliyotokana na shambulizi moja walilolitengeneza langoni mwa Yanga dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Ruvu Shooting walirudi na utulivu uleule huku wakimweka chini ya ulinzi Fiston Mayele ambaye alishindwa kutetema kama ambavyo amefanya kwenye timu nyingine.

“Tulisema tutawabana na nafikiri kila mtu ameona jinsi ambavyo tumecheza na kufanikiwa, tulishasema kuwa Mayele hatatema na kweli, hajatetema sisi sasa tuna timu bora,” alisema msemaji wa Ruvu, Masau Bwire.

Chanzo: Mwanaspoti