Raia wa Nigeria wanaoishi Afrika Kusini wameombwa kuepuka sherehe kubwa na uchochezi endapo ‘Super Eagles’ wataishinda Bafana Bafana. Timu hizo mbili kali za Afrika zitamenyana siku ya Jumatano, ili kumpata atakaye cheza fainali za AFCON 2024.
Wanigeria wanaoishi Afrika Kusini wameshauriwa kuwa waangalifu sana kuelekea mechi ya nusu fainali ya AFCON 2023 kati ya Super Eagles na Bafana Bafana mnamo Jumatano, Februari 7. Katika taarifa yake siku ya Jumanne asubuhi, Kamisheni Kuu ya Nigeria yenye makao yake makuu mjini Pretoria, Afrika Kusini iliwataka raia wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi kuwa makini na lugha wanayotumia kabla na baada ya mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na ghamu na kuwataka kuwa makini kuhusu mahali ambapo watachagua kutazama mchezo huo.
“Kamisheni Kuu ina shauri raia wa Nigeria kuwa makini na matamshi yao, wawe makini na wapi wanachagua kutazama mechi, hasa katika maeneo ya umma na wajiepushe na sherehe za sauti, ghasia au za uchochezi iwapo Super Eagles watashinda mechi.” Ubalozi wa Nigeria ulisema katika taarifa.
Ubalozi ulieleza kuwa tahadhari hiyo inafuatia vitisho vingi vinavyotolewa dhidi ya Wanigeria wanaoishi Afrika Kusini iwapo Bafana Bafana itashindwa na Super Eagles Jumatano usiku.