Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanachotakiwa kufanya Yanga kwa sasa ni hiki

Yanga Hanang Wanachotakiwa kufanya Yanga ni hiki

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

It's Okay malengo ya Yanga yalikuwa ni kutinga hatua ya Makundi Klabu bingwa Africa, yametimia na sasa ni muda wa kupambania bonus.

Kwa sasa ikitokea Yanga ameshinda mechi zake mbili hapa Dar es Salaam basi huenda Yanga ikatinga robo fainal.

Kwa nini?

Kila timu imebakiza mechi 3 ambapo kwa Yanga, mbili anazipiga kwenye Dimba la Benjamin William Mkapa na moja ni pale Misri dhidi ya Al Ahly Sc.

Hesabu zimekaa hivi;

Mechi inayofuata ni Yanga vs Medema huku CR Belouizadad vs Alhy Sc. Yanga Sc akipata ushindi atakuwa na points 5 ambapo kule Algeria itahitajika sare tu kwa CR na Ahly.

Msimamo utakuwa hivi;

Al Alhy Sc 6 Points

CR Belouizadad 5 Points

Yanga SC 5 Points

Medema 4 Points

Belouizadad atakapokuja Dar es Salaam Basi akutane na kipigo hamna namna Huku Al Ahly ashinde au apate sare Nyumbani kwa Medeama pale ghana! Na ikitokea ameshinda Kundi litakuwa hivi

Al Ahly 9 Points

Yanga SC - 8 Points

Belouizadad - 5 Points

Medeama - 4 Points

Mechi ya Yanga na Al Ahly huku Belouizadad na Medeama ndio zitaamua nani aende Robo Fainali! Hapo Belouizadad hata ikitokea ameshinda huku Yanga imepoteza dhidi ya Al Ahly pale Misri atakuwa na Points 8 the same na Yanga Magoli yataamua nani aende

Yanga amecheza mechi 3 ameruhusu goli 5 huku akifunga goli 2 Ana Goli 3 Kama loss Huku Belouizadad amecheza mechi 3 ameruhusu goli 2 na Kufunga goli 4

Yanga -3

Belouizadad +2

Kitu pekee ambacho Yanga tunahitaji kukifanya basi pale Benjamin William Mkapa kila anaekuja apoteze kwa goli nyingi huwenda goal difference ikatumika mwishoni kuamua nani anaenda robo fainali. Kila kitu kinawezekana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live