Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wametumika sana, wanachoshwa

Bruno Fernandez Bruno Fernandez

Sun, 8 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ndiyo maana Bruno Fernandes hafanyi maajabu yake kuokoa jahazi la Manchester United linaloonekana kuzama kila uchao, amechoka!

Nahodha huyo wa Man United, Bruno, 29, alionekana hana kasi ndani ya uwanja katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasary uwanjani Old Trafford Jumatano iliyopita na kuchapwa 3-2, matokeo ambayo yamezidisha presha kwa kocha Erik ten Hag.

Lakini, kwenye kikosi hicho cha Man United, kiungo huyo wa Kireno anaweza kuwa na sababu zinazomfanya ashindwe kufanya vizuri – takwimu zinaonyesha kwamba ndiye mtu aliyecheza sana kuliko mchezaji yeyote kwenye sayari hii kwa sasa.

Takwimu zilizoandaliwa na chama cha kimataifa cha wanasoka FifPro kimefichua kwamba Fernandes amecheza mechi 72 katika miezi 12 iliyopita hadi kufikia Septemba 15 msimu huu.

Hiyo ina maana, Bruno ana wastani wa kucheza mechi moja kila baada ya siku tano, kitu ambacho kwa mchezaji ni mzigo mkubwa.

Kiungo, Fernandes pia anashika namba moja kwa wachezaji waliokuwa uwanjani kwa muda mwingi, akicheza kwa dakika 6,666 katika mechi hizo, ikiwa ni nyingi kuliko mchezaji yeyote.

Baada ya takwimu hizo kuwekwa bayana, mashabiki wa soka walitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii na kutuma meseji zinazoonyesha huruma kwa mchezaji huyo.

“Anahitaji kupumzika,” alisema shabiki mmoja huku mwingine akiandika: “Jamaa, namwonea huruma.”

“Huruma sana,” alisema mwingine na kuongeza: “Bruno ni mashine, lakini mzigo umekuwa mkubwa!”

Kuna huyo aliyesema: “Mungu wangu tunamfanyisha kazi sana, hebu apumzishwe jamani.”

Kuna mwingine alionyesha wasiwasi mkubwa zaidi kwa mkali huyo wa zamani wa Sporting Lisbon, aliposema: “Hii itamletea matatizo ya muda mfupi na mrefu kwenye mwili wake. Anajiweka kwenye hatari ya kupata majeraha makubwa si siku nyingi.”

Hata hivyo, licha ya kutumika sana, mashabiki wanaamini kwamba itakuwa ngumu kwa sasa mchezaji huyo kupewa muda wa kupumzika.

“Hawezi kuwekwa benchi. Yeye ni mchezaji bora kwenye nafasi yake anayocheza kwenye klabu na timu ya taifa,” alisema shabiki mmoja.

Uchovu unaweza kuwa sababu pia inayomfanya mshambuliaji Marcus Rashford, 25, kushindwa kufanya mambo kwenye kikosi cha Man United, ambapo mkali huyo amezidiwa na Fernandes mechi 15 tu. Rashford amecheza mechi 67.

Hata hivyo, kwenye orodha ya mastaa waliotumika sana ndani ya mwaka mmoja uliopita, shida ya Man United inaonekana kuanzia mazoezini kwao kwa sababu mambo ni tofauti huko Manchester City kutokana na kuwa na mastaa waliotumika sana, lakini mambo yao bado ni matamu huko Etihad.

Kuna mastaa wanne wa Man City wamo kwenye orodha ya waliotumika sana, akiwamo Rodri – ambaye hivi karibuni aliadhibiwa kwenye Ligi Kuu England baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa Nottingham Forest, akiwa amecheza mechi 68.

Bernardo Silva yupo mechi moja nyuma, akilingana na Rashford, wakati beki Manuel Akanji akitumika kwenye mechi 66 sawa na straika Julian Alvarez.

Rais wa FifPro, David Aganzo alisema: “Kutumika sana ni moja ya matatizo yanayowakabili wachezaji wanaoshiriki kwenye ligi zenye ushindani mkali.

“Kutokana na ratiba za michuano kuzidi kuongezeka, hakuna namna bora ambayo utawalinda wachezaji wasichoke na kubaki kwenye viwango vyao vya juu kwa muda mrefu.”

Chanzo: Mwanaspoti