Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wametoboa! Tabora United wabaki Ligi Kuu

Tabora United Yabaki .jpeg Wametoboa! Tabora United wabaki Ligi Kuu

Sun, 16 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Tabora United imenusurika kushuka daraja baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa mwisho wa kuwania kubaki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Shujaa wa Tabora United ni mshambuliaji wa Kimataifa wa Angola, Patrick Lembo Aufumu aliyefunga mabao yote mawili, la kwanza kwa penaltı dakika ya 27 na la pili dakika ya 55 akimalizia mpira wa adhabu.

Kwa matokeo hayo, Tabora United inaitoa Biashara United kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza katikati ya wiki.

Ikumbukwe Biashara United imetoka ligi ya NBC Championship ambako iliitoa Mbeya Kwanza katika mchezo na Tabora United ilitolewa na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live