Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wameteka soko la usajili dirisha dogo

Teka Pic Data Dirisha la usajili kufungwa Januari 15

Thu, 30 Dec 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Habari kubwa kipindi hiki cha usajili wa wachezaji katika dirisha dogo lililofunguliwa Disemba 16 mwaka huu likitarajiwa kufungwa Januari 15 mwakani ni namna ambavyo timu mbalimbali zikihaha namna ya kufanya marekebisho ya vikosi vyao kwa kusajili na kuuza wachezaji ili kuhakikisha zinaimarika na kumaliza ligi zikiwa ndani ya malengo yao.

Wakati timu zikipambana kufanya hivyo, baadhi ya wachezaji nao wamezidi kuonesha viwango bora ili kujitafutia soko huku wengi wakipanda bei kutokana na uhitaji wao katika timu nyingine.

Kupitia makala haya, tunakuletea majina ambayo yameteka soko kipindi hiki kwenye Ligi Kuu, Championship, First League na Ligi ya Wanawake.

CLATOUS CHAMA

Ukipita mitaa ya Jangwani na ile ya Msimbazi kipindi huku lazima utakutana na kijiwe cha watu kadhaa wakimzungumzia Mwamaba wa Lusaka, Clatous Chama.

Chama msimu uliopita alikuwa Simba na kuuzwa RS Berkane ya Morroco ambako mambo hayaendi vizuri kwa sasa kwani nafasi yake kikosi cha kwanza imekuwa finyu.

Kiwango alichokionesha Chama kipindi yupo na Simba kimewafanya wababe wa Dar es Salaam, Simba na Yanga kutaka kumrudisha Bongo huku kila mmoja akitamba kumalizana naye licha ya kwamba dalili kubwa zinaonesha kuwa atatua Simba.

METACHA MNATA

WAKATI akiisaidia Polisi Tanzania kuwa katopoteza mechi nane kati ya 10 ilizocheza hadi sasa, kipa huyu wa zamani wa Azam, Mbao na Yanga naye ameliteka soko la usajili kwa sasa.

Kuna tetesi zinaelezwa kuwa mabosi wake wa zamani, Yanga wanahitaji kumrudisha kikosini baada ya kuachana naye msimu uliopita ingawa pia kurudi Yanga inaonekana kuna ugumu kwa pande zote mbili.

Lakini taarifa za ndani zinaeleza kuwa Simba tayari imetuma ofa nono Polisi ikimuhitaji Metacha na kuzua mijadala kibao mtaani kwenye stori za usajili.

CHICO USHINDI

Kiungo Mshambuliaji wa TP Mazembe ambaye kwa sasa ameshika kila eneo wanapozungumza mambo ya usajili.

Ushindi anayemudu kucheza winga zote mbili na straika anahusishwa sana kutua Yanga na taarifa ilizonazo Mwanaspoti ni kuwa mazungumzo yanaendelea baina ya pande zote mbili.

Mkongomani huyu kama atatua Yanga basi ataungana na wakongo wenzake Djuma Shaban, Yanick Bangala, Tunombe Mukoko, Jesus Moloko, Fiston Mayele na Herriter Makambo.

KELVIN YONDANI

Wakati wengine wakisema Yondani ameisha, huko kwenye stori za usajili beki huyu kitasa ndio habari ya mjini.

Yondan ambaye kwa sasa anakipiga Polisi Tanzania amezua mjadala mkubwa baina ya timu yake hiyo na Geita Gold ambao wanamtaka kwa hali na mali.

Inaelezwa kuwa Geita ndio wanaongoza mbio za kunasa saini ya Yondani kwani wameweka mkwanja wa maana mezani na siku yeyote huenda akasaini.

SALUM ABUBAKAR

Mashabiki wa soka nchini humuita ‘Sure Boy’ jina la baba yake mzazi Mzee Abubakar Salum ambalo linachagizwa na ubora wake wa kusakata kabumbu.

Sure Boy tayari amevunja mkataba na Azam FC, timu aliyoitumikia kwa miaka 14 na sasa vigogo wa Kariakoo wanammezea mate.

GERSON FRAGA

Unamkumbuka huyu Mbrazil wa Simba? basi naye huenda akarejea Dar es Salaam na sasa ameliteka soko la usajili akihusishwa kurudi Simba.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa Fraga ameanza mazungumzo na viongozi wa Simba kuhusu kurejea baada ya kuumia kwa kiungo Mganda Taddeo Lwanga ambaye huenda akakaa nje kwa zaidi ya miezi mitano.

ABOUTWALEEB MSHERI

Huyu ni kipa wa Mtibwa Sugar ambaye katika misimu miwili mfululizo ameonekana kufanya vizuri na kufanya jina lake liimbwe kwenye dirisha hili la usajili.

Msheri anahitajika na Yanga lakini inaelezwa kuwa mabosi wa Mtibwa wamemuwekea ngumu licha ya Wanajangwani kuweka dau nono.

Bado mazungumzo baina ya timu hizo mbili yanaendelea na lolote linaweza kutokea.

DENIS NKANE

Kinda huyu kutoka Biashara United, yupo mjini tayari kwa maana ya kila kona unayopita utakuta watu wakimzungumzia.

Nkane ambaye ni kiraka anayeweza kucheza winga zote na beki ya kulia alikuwa anajihusisha kujiunga na Yanga, na tayari amesaini mkataba wa miaka mitatu kinachosubiriwa ni kutambulishwa tu hapo Jangwani.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz