Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wallace Karia, shujaa tusiempenda

Karia Wallace Rais Rais wa TFF, Wallace Karia

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukisikiliza Speech ya Rais wa CAF au ile ya Rais wa FIFA juu ya Wallace Karia na mafanikio aloyapata utaelewa ni kiasi gani hawa jamaa wanamuelewa huyu Mwamba. Karia ameipambania Hela ya FIFA nnma hatimaye amepata cha kuonnesha na WAKUBWA wameona.

Wallace Karia, ni dereva asiyependwa, licha ya mafanikio na ubora wa Uongozi wake lakini bado inamlazimu ajipendekeze ili kuwaridhidhisha WANAFIKI. Karia ameufanyia mpira wetu kila kitu katika dunia ya kisasa, ameupa Heshima na UTAMBUZI lakini “Bingwa la kufeli” anataka kati ya yeye wa KUBWABWAJA na Karia tuchague….. Aonndoke tu.

Wallace hakuwapeleka kina Infantinno Hotel ya nyota kupiga Stori na Mvinyo bali amewapeleka SITE, amewapeleka kule ambapo pesa zimelala, kule kwenye agenda ya maendeleo ya Soka Tanzania kwa mujibu wa FIFA. Karia anaendesha gari lakini kabeba Abiria wasiompenda lakini yeye anachojua ni KUFIKA TU.

Leo kalamu yangu ni HESHIMA FULL TANK Kwa Mwamba wa Mabadiliko na maenndeleo ya Soka la Tanzania. Hatumuimbi kwa sababu hatumpendi na wala picha hizi sio maarufu wala hazitotrend sababu hatumpendi tu na wala hatuna agenda ya kihiiiiivyo ni basi tu Hatumpendi. Binafsi nimeamua kumpa Hadhi anayostahili. NAKUKUBALI MZEE WANGU WALLACE KARIA. .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live