Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wallace Karia: Uwanja wa Mkapa utatumika mechi za Dabi Tu

Wallace Karia Rais wa TFF, Wallace Karia

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Serikali ikijipanga kwa ujenzi wa Viwanja vipya ikiwa ni maandalizi ya AFCON 2027 ambapo Tanbzania itakuwa mwenyeji sambamba na nchi za Kenya na Uganda.

Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) limesema wanafanya jitihada kuhakikisha wanaulinda Uwanja wa Mkapa ili usiweze kuharibika.

Akizungumza Rais wa TFF, Wallace Karia anasema;

“Miundombinu ni jambo ambalo lilikuwa na changamoto sana ,sasa hivi viwanja mmeona vinapendeza lakini uwanja wa Taifa ni uwanja wa serikali. Sisi tunachoangalia ni kuhakikisha uwanja hatuuzidishii matumizi “

“Ikiwezekana ligi zetu ichezwe mechi ya Simba na Yanga tu ,kuhusu ligi mechi zinazoihusu Simba au Yanga zitachezwa sehemu nyingine ,ila wanapocheza wao wenyewe sawa na hata timu ya Taifa tunataka tuangalie sehemu nyingine ya kucheza ili uwanja upumue "

Chanzo: www.tanzaniaweb.live