Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walker ndo basi tena

W640xh480 GettyImages 1469510446 Beki wa Manchester City, Kyle Walker

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa Manchester City, Kyle Walker amezungumza na mabosi wa Bayern Munich kwa ajili ya uhamisho wake kwa sababu kocha Thomas Tuchel ana mipango naye msimu ujao.

Walker aliondolewa kwenye kikosi cha Man City kilichocheza fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Inter Milan, huku tetesi zikiripoti beki huyo wa kimataifa wa England ataondoka kikosini hapo katika dirisha hili la usajili wa kiangazi.

Kituo cha televisheni cha Sky Sports kutoka Ujerumani kimeripoti kwamba yalikuwepo mazungumzo kati ya mabosi wa Bayern na wawakilishi wa Walker, lakini klabu bado hazijafikia makubaliano kuhusu uhamisho.

Inadaiwa kwamba Walker ameonyesha nia ya kujiunga na Bayern kwa sababu kocha wa Man City, Pep Guardiola hana mipango naye msimu ujao baada ya kumtema kikosini kwenye fainali. Ripoti ya Sky Sports imeeleza kuwa: "Pande zote mbili zinaamini dili litakamilika, huku Man City wakisaka beki mwingine atakayeziba pengo la Walker."

Gazeti la Mail limeripoti kwamba Sheffield United ina mpango wa kumnyakuwa Walker na kumrudisha katika klabu yake ya zamani, licha ya kuhusishwa na Bayern ambayo itamwezesha kucheza michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya msimu ujao. Wakati huohuo, Sheffield United ipo tayari kumkaribisha Walker nyumbani kwa mara nyingine baada ya kuondoka 2009. Klabu hiyo inataka kuimarisha kikosi baada ya kurejea Ligi Kuu England.

Baada ya kuondoka Sheffield, Walker alijiunga na Tottenham Hotspurs kabla ya kutua Manchester City 2017. Walker amecheza mechi 250 tangu alipotua Etihad na kubeba mataji 12 yakiwemo matano ya Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hivi karibuni aliweka wazi kwamba alichukizwa na kitendo cha Guardiola kumuweka benchi kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

"Ilinishangaza sana, lakini ndoto yangu ikatimia na tukabeba ubingwa. Tulipambana sana kupata mafanikio kwa muda mrefu kubeba makombe matatu sio mchezo," alisema Walker.

Chanzo: Mwanaspoti