Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walitajwa kutua Simba, Yanga dirisha dogo, wameyeyuka kusikojulikana!

MASTAA ER Magazeti

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza kufunga rasmi dirisha dogo la usajili kwa msimu wa 2022/23.

Wakati wa kufunguliwa kwa dirisha hilo majina ya nyota mbalimbali yalihusishwa kutua nchini kwaajili ya kuja kukipiga kwenye NBCPL lakini mpaka usajili unafungwa majina hayo hameota mbawa na kubakia kuwa stori za kisadikika mpakawisho wa msimu huu wa 2022/23.

Majina hayo ni pamoja na Bobos Byaruhaga ambae alitajwa kuwa atajiunga na Yanga lakini mwisho wa siku ametimkia nchini Marekani.

Si hivyo tu pia baadhi ya maofisa wa Yanga walianza kueneza taarifa kuwa Luis Miquissone ambae aliwahi kukipiga kwenye klabu ya Simba kuwa atajiunga na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili lakini mwisho wa siku amebaki aliko.

Kwa upande wa Simba jina la Cezar Manzoki limekuwa likitajwa toka wakati wa dirisha kubwa la usajili 2022/23 kuwa atajiunga na Simba lakini baadaye dili lake lilibuma na akatimkia nchini China.

Katika dirisha hili dogo, Manzoki kulikuwa na taarifa kuwa nyota huyo yupo kwa mkataba wa muda mfupi na wakati wa dirisha dogo atajiunga na Wekundu wa Msimbazi lakini mwisho wa siku naye amesalia China na ku kusalia kuwa ni stori ya kusadikika mpaka wakati mwingine,

Kwa upande wa Makusu Mundele nae pia dili lake la kuinunga na Mnyama limegonga mwamba kutokana na kuwa, nyota huyo ameshacheza Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na FC Lupopo hivyo itakuwa ni vigumu kwa Simba kumtumia kwenye michuano hiyo kwa mujibu wa sheria zinavyoelekeza.

Usajili gani umekuvutia (Yanga & Simba) hadi sasa kwenye dirisha dogo 2022/23?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live