Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walipofikia Yanga siwadai - Shaffih Dauda

Skudu Moloko Kibabage Sure Boy Kibwana Yanga Kikosi cha Yanga.

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi nguli wa masuala ya soka nchini, Shaffih Dauda amesema kuwa kuwa kwa walipofikia Klabu ya Yanga kwenye michuano ya kimataifa, yeye hawadai kwani wamefanya kila kitu kwa level yao.

Ikumbukwe kuwa, Yanga mpaka sasa wamefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya miaka 25, huku wakicheza michezo minne ya hatua hiyo wakishinda mmoja, sare mbili na kufungwa mchezo mmoja.

Yanga wapo nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi lao wakiwa na alama 5 sawa na Al Ahly ambao wao wamecheza mechi tatu.

“Mimi ukiniuliza walipofika Yanga sasa hivi na walipo Simba SC, Yanga siwadai kwa kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ni mafanikio kwao,mwaka jana wamecheza fainali ya CAFCC kwangu mimi kuna ukuaji kutoka Shirikisho hadi Klabu bingwa makundi”

“Nikiangalia walipotoka na jinsi wanavyoenda wamemaliza siwadai,” amesema Shaffih Dauda.

Una maoni gani?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live