Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliosema 'Kombe la Luza' wamesherekea medali mpaka Ikulu - Saleh Jembe

Yanga Mreee Waliosema 'Kombe la Luza' wamesherekea medali mpaka Ikulu - Saleh Jembe

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini Saleh Ally Jembe amesema kuwa wapo baadhi ya viongozi na mashabiki wa soka nchini ambao wamekuwa wakibeza baadhi ya mashindano wakidai kuwa ni hadhi ya chini.

Bila kutaja majina, wakati akihojiwa hivi karibuni, Jembe ametolea mfano waliowahi kusema kuwa michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ni ni ya wale walioshindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Mabingwa wa Afrika na kuangukia Shirikisho.

"Hao waliosema kombe la 'luza' si ndio hao wamelishangilia wakaimba na kurukaruka. Kombe la Shirikisho lina heshima yake ndio maana Yanga wamepeleka Medali hadi Ikulu, umewahi kuona watu wanashangilia medali ya mshindi wa pili?

"Kwa hiyo hata wao wamefurahia, ikitokea mtu anakwambai kombe la shirikisho halina maana ujue huyo hajitambui.

"Kombe la Shirikisho na Klabu Bingwa Afrika kila moja ina hadhi yake, zinashiriki timu kubwa zenye historia kubwa ya kuchukua ubingwa wa michuano mkubwa Afrika, ingekuwa hii michuano ni ya hovyo basi watu wasingekaribishwa Ikulu.

"Tanzania ikitokea timu ikachukua ubingwa wa shirikisho, itakuwa rekodi ya kwanza kwa sababu haijawahi kutokea. Nadhani tutafanya maandamano makubwa sana kama mshindi wa pili tu tulifanya maandamano makubwa vile," amesema Jembe.

Ikumbukwe kuwa, Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara aliwahi kunukuliwa akiwaponda wapinzani wao Simba kwa kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na kudai kuwa ni Kombe la walioshindwa 'luza'.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: