Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walion'goa viti mechi ya Yanga kushughulikiwa - MwanaFA

MWANAFA BASATA Walion'goa viti mechi ya Yanga kushughulikiwa - MwanaFA

Mon, 4 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu waziri, Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Hamis Mwinjuma 'MwanaFA' ameuhakikishia umma wa Watanzania kuwa waliofanya uharibifu kwenye mchezo wa Klabu bingwa Afrika (CAFCL) kati ya Yanga na Al Ahly watachukuliwa hatua kama walivyochukuliwa hatua waliofanya uharibifu mwaka 2016 kwenye mchezo wa derby ( Simba VS Yanga) uliomalizika wa sare ya 1-1.

Mwinjuma amesema kitendo hicho hakivumiliki na hakikubaliki hivyo waliofanya hivyo lazima wagharamie.

"Ule ni uhuni kama uhuni mwimgine, kama ilivyotokea wakati ule wa dabi ya Simba na Yanga, lazima walipe," alisema Mwinjuma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live