Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliomwacha Msuva wanamtaka Sergi Roberto

Sergi Roberto Es Sergi Roberto.

Fri, 1 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa tovuti ya Mundo Deportivo, Al Qadsiah ya Saudi Arabia aliyowahi kuichezea Mtanzania Simon Msuva, imemwekea mezani ofa nono kiungo na nahodha wa Barcelona, Mhispania, Sergi Roberto ili ajiunge nao dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Licha ya ofa hiyo ripoti zinadai staa huyu amekataa na kuonyesha nia ya kutua Marekani badala ya Saudia.

Roberto mkataba wake wa sasa unamalizika mwisho wa msimu huu na anahusishwa kuwa kwenye mpango wa kuondoka kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya.

Al Qadsiah inataka kumsajili staa huyu ikiwa ni sehemu ya mipango ya kocha wao Michel aliyewahi kuhudumu kwenye benchi la ufundi la Real Madrid kuanzia timu za vijana hadi wakubwa akiwa kama msaidizi.

Kocha huyo anamtaka Roberto ikiaminika ataenda kuisaidia timu kupanda daraja kwenda Ligi Kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live