Mon, 10 Jun 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mashabiki watatu wa Timu ya Valencia waliombagua Staa wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Brazil Vinicius Junior (23) wamehukumiwa kifungo cha miezi 8 jela.
Mashabiki hao pia wamepewa adhabu ya kufungiwa miaka miwili kuingia viwanjani kutazama mechi Nchini Hispania, baada ya kukutwa na hatia ya kosa walilotenda Mei 2023 katika uwanja wa nyumbani wa Valencia unaojulikana kwa jina la Mestalla wakati wa mchezo dhidi ya Madrid.
Habari hii imekuwa kubwa zaidi Nchini Hispania kwasababu ndio mara ya kwanza Shabiki wa soka kupata hukumu kubwa ya kosa la ubaguzi wa rangi.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live