Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amewapiga kijembe watani zao wa jadi, Yanga Sc baada ya kushinda Ubingwa wa Ngao ya Jamii.
Huu ni mwendelezo wa Ahmed kuwazodoa majirani zake hao na ametupa kijembe hicho leo ikiwa ni takribani wiki 2, tangu Yanga wapoteze mchezo huo kwa mikwaju penati 3-1.
"Mahaba ya mimi ya kuwaondolea maumivu Yanga, Mimi na Ally Salim tutaenda Avic Town, mimi nitabeba Ngao ya Jamii na Ally Salim atabeba Gloves, halafu wale wachezaji wa Yanga waliokosa penati warudie kupiga penati kuanzia asubuhi mpaka jioni, wakishinda tunawaachia Ngao ya Jamii," amesema Ahmed Ally.