Hatua ya 16 bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup imekamilika jana kwa michezo miwili ambapo klabu za Simba SC na Pamba FC zimeungana na timu nyingine 6 ambazo zilishafuzu hatua inayofata ya robo fainali.
Jana Pamba FC na Simba zilishinda michezo yao na kufuzu hatua ya robo fainali ambapo klabu ya Pamba ya Mwanza ilikata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali baada ya kuifunga Dodoma Jiji FC mabao 2-1 na kuifanya timu hiyo kuwa ndio timu pekee kutoka Championship kusalia kwenye michuano hii kati ya timu 8 huku timu 7 zikikiwa ni za Ligi Kuu.
Timu ya Pamba FC ni timu pekee iliyofuzu hatua ya robo fainali ambayo sio timu ya Ligi Kuu
Simba ambao ni mabingwa watetezi wao ndio walikamilisha hatua ya 16 kwani mchezo wao ulikuwa wa mwisho ulichezwa kuanzia majira ya Saa 1:00 Usiku, na wakufuzu kwa ushindi wa mabao 7-0 wakiinyuka Ruvu Shooting.
Baada ya michezo hiyo miwili ya Jana imekamilisha timu 8 zilizofuzu hata ya robo fainali ambapo Simba SC mabingwa watetezi wa michuano hii kwa misimu miwili mfululizo wanaungana na , Azam FC, Yanga SC, Kagera Sugar, Coastal Union, Geita Gold, Pamba FC na Polisi Tanzania.