Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walichofaulu Ihefu kwa Yanga ni hiki

Ihefu Yanga Ns Walichofaulu Ihefu kwa Yanga ni hiki

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Stephen Abissay amesema kuwa walichokiweza Ihefu FC kwa Yanga ilikuwa ni kasi kubwa wakati wakifanya counter attack ya haraka iliyozaa bao kipindi cha pili.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa jana katika Dimba la Southern Highland huko Mbarali, mkoani Mbeya, Ihefu kwa mara nyingine ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Yanga.

"Kwenye scenario ya goli la pili, wakati wa ile Counter attack Ihefu walibadilishana mpira haraka kwa pasi chache almost 3 tena kwa speed ukizingatia Mahundi ana kasi sana.

"kwa hiyo ukisimamisha ile video ya wachezaji wa Yanga wakati Mahundi yupo kule juu, kuna wachezaji 8 wa Yanga wanarudi kutoka eneo moja kwenda lingine sio kwa kasi ile "they are jogging" wanarudi kwenye eneo lao,"

"Lakini Ihefu walikuwa na speed zaidi ya kukimbia tu as a player lakini hata kubadilishana ule mpira, ni kana kwamba plan yao kabisa ilikuwa hiyo kwamba ili umfunge Yanga "they have to work speedly more than them" wawahi kufika kwenye eneo sahihi na ndicho ambacho kilitokea," amesema Abissay Stephen.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: