Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walichofanyiwa na Simba... Mashujaa walia usalama mdogo Chamazi

Mashujaa Dsc Mashujaa walia usalama mdogo Chamazi

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwenye mchezo wa Ligi kuu kandanda Tanzania Bara jana kati ya Simba dhidi ya mashujaa uliomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli 2-0 kuna tukio lilitokea la shabiki kuingia uwanjani kwenye lango la Mashujaa fc na kisha kuanza kufanya yake pale langoni.

Wadau wengi kwa namna tofauti wameonyesha kushangazwa na kile kilichotokea akiwemo himid mao Mkami nyota wa zamani wa Azam fc ambaye kwasasa ana kipiga nchini Misri.

Mao aliandika “Huu ni ushenzi haijalishi nani anaenda kutoa hayo mataulo ya magolikipa golini, very unprofessional kwenye dunia ya sasa mchezaji au shabiki kwenda kutoa mataulo na maji kwenye ligi inayoonyeshwa kwenye Tv it’s very sad na watu wanachekelea haya mambo”.

Baada ya maoni mengi ya wadau kulalamikia suala hili ikiwemo pia ulinzi kutokuwa imara daudasports ikamtafuta afisa habari wa bodi ya Ligi karimu Boimanda ambaye alitolea ufafanuzi juu ya jambo hilo akieleza kuwa sheria itachukuliwa kwa kila aliyehusika na amekiri kutokea kwa uzembe wa maafisa usalama wa mchezo huo.

“Kanuni za Ligi zinakataza hayo mambo, wanaofanya wanazifahamu, Kama waliohusika watathibitika wamefanya makosa kanuni zipo, zinawagusa wadau wote.”

“Aliyefanya hilo tukio ni shabiki, kwasasa hivi tunaavyo zungumza hauwezi kujua ni shabiki wa timu gani, kwahiyo siwezi kusema nani na nani ataenda kuadhibiwa kwenye hilo jambo ni kanuni tu.”

“Kuna kikao cha kamati ya usimamizi na uendeshaji wa Ligi, ndio kitajadili hayo mambo, kufuata kanuni.”

– Karimu Boimanda, Afsia Habari wa Bodi ya Ligi kuu Tanzania

Kwa upande wa klabu ya Mashujaa kutoka Mkoani Kigoma kupitia kwa Mwenyekiti wake Maj Tak wameeleza kuwa kwasasa wanaandika Barua kuelekea Bodi ya Ligi juu ya kile kilichotokea jana na kama usalama ni mdogo pale Azam Complex basi ufungiwe kutumika uwanja huo.

“Tumedhamiria kuandika barua ya malalamiko kwasababu kama uliangalia vizuri, kabla ya tukio lile mechi ilikuwa bila bila, wachezaji wangu na kipa wakatoka mchezoni.”

“Tunaandika barua pia kuhusu uwanja wa Azam, kama usimamizi haupo basi nao ufungiwe, malalamiko yetu yanaegemea kwenye usalama wa wachezaji.”

“Hata mechi ya Yanga hivyo hivyo, kuna mtu alienda akatoa taulo la golikipa wetu, sijui kama sisi mashujaa ndio wachawi sijui, wakati mambo haya mimi nayakemea kila siku kwenye timu yangu, lakini nashangaa leo watu wanafanya mambo ya ajabu.”

“Mimi huwa naamini kwenye timu bora, timu ikiwa nzuri mambo ya ushirikina huwa hayana nguvu, ni kweli vipo lakini mimi huwa navipinga sana yani.”

“Michezo mingi huwa inatokea, kwasisi hapa mashujaa imetokea mara nne, ushauri wangu ni kuwa tuache mambo ya kishirikina, timu zikiwa nzuri unashinda tu.”

Mwenyekiti wa klabu ya Mashujaa kuhusu kilichotokea Chamazi kwenye mchezo wao dhidi ya Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live