Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waleteni tuwafundishe soka kwa Mkapa

Azam FC Kuendelea Kuchezea Kichapo Kwa Yanga Jumapili Waleteni tuwafundishe soka kwa Mkapa

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu ya soka Tanzania bara inaendelea tena leo Oktoba 23, 2023 kwa mechi moja ambapo Mabingwa watetezi, Yanga SC watakuwa wenyeji wa Azam FC katika dimba la Benjamin Mkapa kwenye Derby ya Mzizima majira ya saa 12:30 jioni.

YANGA SC vs AZAM FC

Benjamin Mkapa

Saa 18:30 jioni.

Azam FC inaingia katika mechi hii ikiwa mnyonge wa Wananchi baada ya kushindwa kupata ushindi katika mechi 5 zilizopita sare moja na vipigo vinne.

Katika mechi mbili zilizopita Azam FC ilipoteza 2-0 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii mnamo Agosti 9, 2023 na kipigo cha 3-2 kwenye Ligi Kuu msimu uliopita mnamo Disemba 25, 2022.

Chachu ya mchezo huu inakuja pale ambapo yeyote atakayeshinda atakwea kileleni mwa msimamo wa NBCPL. Azam FC inakamata nafasi ya pili alama 13 baada ya mechi 5 huku Yanga ikishikilia nafasi ya tatu alama 12 baada ya mechi 5.

Kinara Simba SC hajapoteza mchezo wowote baada ya kukusanya alama zote 15 kwenye mechi zake 5 za mwanzo.

Je, Wanalambalamba watafuta uteja mbele ya Mabingwa watetezi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: