Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waletee Simba na Yanga

MAYELE PHIRII Waletee Simba na Yanga

Sat, 11 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Simba inaanza leo, Yanga kesho kwenye mechi za awali za makundi za michuano ya CAF. Wekundu wa Msimbazi wapo Guinea kutupa karata ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikiwa Kundi C kwa kuuamana na AC Horoya mjini Conakry.

Baada ya hapo itakuwa ni zamu ya Yanga mjini Tunis, Tunisia kuvaana na US Monastir katika mechi ya Kundi D ya Kombe la Shirikisho Afrika. Makundi sio rahisi

Katika droo ya Desemba 12, mwaka jana iliyoendeshwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), timu hizo zilijikuta kwenye makundi ambayo huwezi kuyaita kama ni mepesi ama magumu, ila itategemea na wawakilishi hao hao watazichanga vipi karata za mechi hizo.

Mbali na Raja na AC Horoya Kundi la Simba lina Vipers ya Uganda ambayo jana Ijumaa ilikuwa ugenini kuvaana na Wamorocco, ilihali Yanga ipo kundi moja na Rela Bamako ya Mali ambayo itaanza mechi zake ugenini dhidi ya TP Mazembe.

Hii ni mara ya tatu kwa Yanga kucheza Makundi ya Shirikisho baada ya mwaka 2016 na 2018 wakati Simba ni mara ya tatu kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya 2003, 2018-2019 na 2020-2021 huku mara mbili zilizopita ikifika robo fainali.

Kwa msimu uliopita wa michuano ya CAF, ilicheza makundi na kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kuondoshwa Ligi ya Mabingwa na Jwaneg Galaxy ya Botswana.Licha ya rekodi tamu kwa Simba na hata kwa Yanga kulinganisha na wapinzani wao wengine ukiondoa Raja na Mazembe, bado wawakilishi hao wana kazi ngumu kwenye hatua hiyo ya makundi ambayo hutoa washindi wawili wa kila kundi kutinga robo fainali.

Minoti ya kutosha Ukiondoa kila timu kutaka heshima kwenye michuano hiyo, lakini uwepo wa zawadi nono za washindi wanaoenda robo fainali na hatua za juu ikiwamo mabingwa, ndio inayofanya mechi za makundi kutokuwa lelemama.

Simba kwa kutinga makundi ya Ligi ya Mabingwa imejihakikishia Dola za Kimarekani 550,000 (karibu Sh1.2 bilioni) hata kama itashindwa kwenda robo fainali. Ikifika robo fainali basi itabeba Dola 650,000 (Sh1.5 bilioni).

Ikifika nusu fainali basi itazoa Dola 875,000 (Sh2 bilioni) na ikimaliza kama mshindi wa pili itavuna Dola 1,250,000 (zaidi ya Sh2.8 bilioni) na kama itabeba ubingwa itanyakua Dola 2,500,000 (zaidi ya Sh5.7 bilioni).

Yanga kwenye mechi zao za Kombe la Shirikisho nako ni mwendo wa fedha tu, ilimradi yenyewe iamue kuishia njiani, lakini ikiwa tayari imeshavuta kibunda cha Dola 275,000 kwa kutinga makundi ya michuano hiyo. Kiasi hicho cha fedha ni zaidi ya Sh630 milioni).

Kama itafika robo fainali basi itavuna Dola 350,000 (zaidi ya Sh800 milioni) na ikitinga nusu mzigo utafikia Dola 450,000 (zaidi ya Sh1 bilioni) na ikimaliza kama mshindi wa pili basi itavuta Dola 625,000 (zaidi ya Sh1.4 bilioni) na ikibeba ndoo itaondoka na Dola 1.25 milioni (zaidi ya Sh2.8 bilioni).

Wapinzani washinde

AC Horoya inayokata utepe na Simba leo mjini Conakry huu ni msimu wao wa 13 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, mafanikio makubwa kwao ni kufika robo fainali mwaka 2018 na 2019 na msimu uliopita iliishia makundi tu. Lakini ndio Mabingwa wa Kombe la Washindi Afrika mwaka 1978, ikiwa na miaka mitatu tu tangu klabu ilipoasisiwa 1975.Ndio timu kinara wa soka la Guinea na ina nyota wakali ambao Simba ni lazima iwe macho nao hasa eneo la kiungo wanapoupiga mpira mwingi, ikifundishwa na Kocha Lamine Ndiaye, nyota wa zamani wa Senegal.

Baadhi ya nyota wake ni Mohamed Camara, Abou Mangue, Issaka Samake, Boubacar Samassekou, Ibrahima Doumbouya, Salif Coulibaly, Khadim Diaw, Fode Camara, Baffour Sebe, Mory Kante, Ocansey Mandela, Mohamed Djibo, Ismael Camara, Daouda Camara, Sory Traore na Alseny Soumah.

Raja Casablanca

Imetwaa ndoo ya Afrika mara tatu kwenye miaka ya 1989, 1997 na 1999 kwa sasa ina njaa ya zaidi ya miaka 20 bila ya Kombe la Ligi ya Mabingwa hilo ambalo kwenye miaka ya hivi karibuni imekuwa ikiishia hatua ya robo, nusu na fainali.

Raja imebeba pia Kombe la Shirikishi mara mbili 2018 na 2021, huku ikibeba CAF Super Cup 2000 na 2019 na lile la Kombe la CAF 2003 ambalo Simba iliwahi kufika fainali mwaka 1993. Kwa sasa inanolewa na Mondher Kabaier, sio timu ya kubezwa na Simba lazima ikaze buti itakapovaana nao wiki ijayo.

Vipers

Awali walifahamika kama Bunamwaya kabla ya kubadilisha jina Agosti mwaka 2012 na kuwa Vipers. Ilitinga makundi ya shirikisho ikiwa na Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’.

US Monastir

Kwa upande wa wapinzani wa Yanga kwenye Kombe la Shirikisho. Ilianzishwa Machi, 1923 lakini ikiwa haina maajabu sana kwenye michuano ya CAF, kwani inashiriki mara ya kwanza kwenye makundi ya Shirikisho.

TP Mazembe

Hii ndio timu kigongo kwa Yanga kutokana na historia yake kwenye michuano ya CAF, kwani mbali na kushiriki mara 25 Ligi ya Mabingwa Afrika, imebeba ndoo mara tano na kwenye Shirikisho huu ni msimu wa nane kwao, ikibeba mataji mara mbili 2016 na 2017.Timu hizo sio ngeni kwenye michuano hio kwani zilishakutana kwenye hatua kama hiyo mwaka 2016 na Yanga ilichezea vichapo nje ndani ikianza kufungwa nyumbani bao 1-0 kisha kulala tena ugenini kwa mabao 3-1.

Real Bamako

Huu ni msimu wake wa nne kushiriki shirikisho mara ya mwisho ilicheza makundi 2014, lakini ikitangulia kutolewa raundi ya awali mwaka 2011 na 2012 iliishia raundi ya pili.Rekodi yake tamu ipo kwenye Ligi ya Mabingwa ikicheza mara 10, ikimaliza mshindi wa pili mwaka 1966, miaka sita tangu ilipoasisiwa baada ya kufika fainali na mwaka 1982 ilifika robo fainali hatua ya juu zaidi tangu fainali ya 1966 na mara ya mwisho kushiriki Kombe la Shirikisho 2018, Kombe la washindi imecheza mara mbili 1990 na 1997.

Chanzo: Mwanaspoti