Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wales yafuzu Kombe la Dunia baada ya Miaka 64

Wales+win Wales yafuzu Kombe la Dunia baada ya Miaka 64

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wales imeafnikiwa kufuzu kushiriki kombe la Dunia 2022 nchini Qatar baada ya kufunga Ukraine 1-0 siku ya Jumapili katika mchezo wa mchujo ambao ulicheleweshwa sababu vita inayoendelea nchini Ukraine.

Imepita miaka 64 tangu Wales wacheze michuano ya Kombe la Dunia mara ya mwisho ilikuwa kombe la Dunia la mwaka 1958.

Goli la kujifunga la Andriy Yarmolenko ambaye alikuwa akijaribu kuokoa mpira uliyopigwa na Gareth Bale lilitosha kuivusha Wales ambao walikuwa wakiota kila mara kushiriki michuano hiyo mikubwa katika ulimwengu wa soka.

“Ni matokeo bora zaidi katika historia kwa soka la Wales,” Bale aliambia Sky Sports. “Sote tuna furaha. Mashabiki kwa pamoja, ilikuwa furaha, na tunaenda kwenye Kombe la Dunia!

“Inamaanisha kila kitu. Ndivyo ndoto zinatimizwa. Ndio tumekuwa tukifanya kazi tangu tulipokuja hapa. Nina furaha kwa mashabiki wetu wote wa ajabu na nchi yetu. Maneno hayawezi kuelezea jinsi tunavyojisikia. kwa sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live