Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakongwe wafurika tuzo TFF

Wakongwe Pic Data Wakongwe wafurika tuzo TFF

Fri, 22 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Nyota wa zamani wa soka wamejitokeza kwa wingi katika hafla ya tuzo za TFF inayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam.

Idadi kubwa ya wachezaji hao ni wale waliochezea Simba na Yanga miaka ya nyuma ingawa wapo waliowahi kutamba katika timu nyingine

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF, James Mhagama aliyewahi kuchezea Majimaji ya Songea ni miongoni mwa nyota wa zamani waliojitokeza katika hafla hiyo

Nahodha wa zamani wa Yanga, Ally Mayay naye pia yupo katika hafla hii huku pia akiwepo nyota wa zamani wa Simba, Abdallah Kibaden aliyeshinda tuzo ya gwiji wa soka.

Pia wapo Abeid Mziba, Ramadhan Kampira, Madata Lubigisa, Hery Morris na Mohamed Mwameja

Wengine ni Mohamed Muharami, Jemedari Said na Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao aliyewahi kuchezea Simba

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz