Kuna jambo tunaweza kujifunza kuwa, wachezaji kutoka DR Congo wamekuwa na mafanikio makubwa katika misimu hii miwili au mitatu ya ligi yetu au msimu kwa ujumla.
Mafanikio yao ni kwa mabeki, viungo na washambulizi. Tuzo ya beki bora, mchezaji bora ilienda kwao, pia mfungajj bora wa pili akibeba Mayele nyuma ya George Mpole.
Msimu uliomalizika; mchezaji bora, mfungaji bora, wamo kwenye kikosi bora na kadhalika. Bila shaka wamekuwa sehemu ya changamoto kuanzisha na kuendeleza ushindani.
Yanga ndio wamefanikiwa zaidi kupitia wachezaji kutoa taifa jirani lakini Simba na hata Azam FC.
Kweli kuanguka kwa TP Mazembe, pia AS Vita kimataifa, kumeshusha kiasi thamani yao lakini, DR Congo ni bora zaidi yetu kwa vipaji, au wanajituma sana utayari wa kutotaka kurudi tena nyumbani wakiwa wameshindwa?